UKAWA WATANGAZA MAJIMBO WALIYOGAWANA KATIKA UCHAGUZI MKUU

 Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi,  Nderakindo Kessy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi Makunjunga.

Continue reading “UKAWA WATANGAZA MAJIMBO WALIYOGAWANA KATIKA UCHAGUZI MKUU”

Advertisements

NYERERE: WAZEE NDIO NGUZO YA NCHI

Nyerere na mama yake Bi Mgaya pamoja na mkewe

Mwalimu Nyerere akiwa na mama yake mzazi, Bi Mgaya (kushoto) na mkewe Bi Maria Nyerere mwaka 1993.

Na Daniel Mbega
DEMOKRASIA ya sasa imepanuka kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma, hasa kipindi cha ukoloni. Leo hii tunashuhudia hata vijana wa shule wanaifahamu vyema siasa, huku uongozi ukishikwa na vijana wadogo, wengine wakiwa hawajafikisha hata miaka 30.
Mwaka huu tunapomuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo chake, tumeona bora tuzungumze, na tulete hotuba yake, akielezea namna alivyoanza siasa miaka ile ya 1950, mara baada ya kurejea kutoka mamsomoni Scotland.
Yeye anasema kwamba alianza akiwa ‘mdogo’ akiwa na miaka 30 hivi mwaka 1952 aliporejea, lakini kwa sasa ukitaja miaka hiyo huwezi amini kama hukuwakuta waheshimiwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hata wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa wametopea kweli kwenye siasa.
Kwa miaka ile umri huo alikuwa bado mdogo, na hata yeye mwenyewe anakiri kwamba alikuwa kijana mdogo.
Hata hivyo, Mwalimu aliamini kwamba wazee ndio nguzo ya maendeleo ya nchi, kwani yeye mwenyewe asingeweza kufanikiwa kama si kulelewa na wazee waliompa miongozo ya kutosha hadi akafikia mahali alipofikia.
Mwalimu aliyasema haya mbele ya Baraza la Wazee wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiagana nao kabla ya kung’atuka mwaka 1985. Hebu tuungane…
“MIMI nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

NYERERE ALISEMA, UJAMAA HAUKUSHINDIKANA…

nyerere_and_sokoine

Na Daniel Mbega

KAMA kuna kitu ambacho Mwalimu Nyerere alikiabudu – mbali ya Mungu kupitia katika imani yake ya Kikatoliki – ni Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliyozaliwa ndani ya Azimio la Arusha, ambayo aliendelea kuihubiri na kuitetea kwa nguvu zake zote hadi kikomo cha uhai wake.

Kila alikokwenda daima alitembea na Biblia pamoja na Azimio la Arusha, akiamini kwamba misingi ambayo TANU iliiweka kwenye azimio hilo Februari 5, 1965 pale Arusha ilikuwa mizuri na ingeendelea kuwa mizuri ikiwa tu Watanzania wangemwelewa dhamira yake.

Azimio la Arusha lililohimiza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea bado liko katika maandiko, ikiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ingawa kwa sasa ni nadharia tu na si vitendo.

Hii inatokana na azimio hilo ‘kuuawa’ na Azimio la Zanzibar la mwaka 1991, ambalo lilileta ‘Soko Huria’ enzi za Awamu ya Pili ya uongozi chini ya Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambaye alitoa ruksa kwa kila kitu, zikiwemo nguo za mitumba (maarufu wakati huo kama ‘kafa Ulaya mazishi Bongo’).

Soko huria hili likatafsiriwa vibaya na watu wengi, wakiwemo watumishi wa umma ambao enzi zile za Mwalimu na siasa yake ya ujamaa na kujitegemea walijiona wameminywa, sasa wakaachana hata na misingi ya utawala bora na maadili ya uongozi wa umma, pamoja na miiko ya viongozi, na kuamua kujilimbikizia mali kadiri walivyotaka kwa kutumia nyadhifa zao, jambo ambalo TANU, na baadaye CCM, ililikemea kwa nguvu zote.

Kwa zaidi ya miaka 24 chini ya utawala wa Mwalimu Nyerere, Tanzania iliishi chini ya mfumo wa Ujamaa, siasa ambayo iliweka njia zote kuu za uchumi chini ya umiliki wa umma, ambapo wengi wanasema hali hiyo ndiyo ilichelewesha maendeleo kwa Tanzania.

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, alikaririwa Julai 2008 akisema kwamba ujamaa ulikuwa hautekelezeki.

Ujamaa ni siasa nzuri lakini unapingana na uasili wa binadamu. Watu, wakati wote wanapenda kuwa matajiri. Hawataki kuwa maskini kwa maisha yao yote. Msingi mmoja wa ujamaa ni kwamba kusiwepo na pengo kubwa kati ya matajiri na maskini, pengo ambalo sasa tunalishuhudia huku wachache wakiwa wamejilimbikizia mali kinyume cha utaratibu na wakitamani kuendelea kuchota mali za umma na hata kununua uongozi au madaraka ili waendelee kuifaidi keki ya fursa za kiuchumi huko walio wengi wakiendelea kuogelea katika ufukara wa kutisha.

SOMA ZAIDI:http://brotherdanny5.blogspot.com/2013/10/nyerere-alisema-ujamaa-haukushindikana_14.html

 

NYERERE ALIHIMIZA ‘ELIMU NI KAZI’

Nyerere na baiskeli
Na Daniel Mbega

“VIJANA wetu lazima wapate elimu inayoendana na Afrika. Hii ina maana kwamba, elimu ambayo siyo tu inatolewa Afrika lakini pia inayolenga kukidhi matakwa ya sasa ya Afrika.” Hayo ni maneno aliyoyatoa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Oktoba 25, 1961 akizungumzia kuhusu elimu na sheria.

Leo tunapokumbuka miaka 14 ya kifo chake tunaona fahari kubwa kukumbuka maneno ya busara ya Mwalimu Nyerere, ambaye siyo tu alisukumwa na taaluma yake ya ualimu, bali nia yake ya dhati ya kuhakikisha kwamba elimu bora inatolewa kwa kila mtu.

Mwalimu Nyerere aliamini kwamba, elimu pekee ndiyo ingeleta maendeleo ya Tanzania, na hata Afrika kwa ujumla, na ndiyo maana hata katika hotuba zake nyingi alisisitiza umuhimu wa watoto kufundishwa namna ya kujitegemea na siyo kufaulu mitihani tu.

Mwalimu aliamini kwamba elimu ni ule ujuzi ambao unamwezesha mtu kujitegemea katika mazingira yanayomzunguka, na siyo fikra zile za kale za kuona kwamba eti mtu mwenye elimu mahali pake pa kazi na ofisini tu.

SOMA ZAIDI http://brotherdanny5.blogspot.com/2013/10/tunapomsimanga-mwana-pekee-wa-nyerere_14.html

MWALIMU NYERERE, WENZIO WANAUVUNJA MUUNGANO!

Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume

Na DANIEL MBEGA

Salaam Mwalimu Nyerere,
Sina shaka kwamba huko uliko umepumzika kwa amani, kwa uwezo wa Mungu. Yawezekana umekuwa mwenyeji huko na kazi yako njema uliyoifanya katika kuhakikisha Tanganyika inajitawala, na hatimaye inaungana na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kuzaa Tanzania, bado ni kitambulisho tosha ndiyo maana leo hii, miaka 14 baada ya kifo chako, bado Watanzania tunakukumbuka huku duniani.
Lakini nina uhakika hujui yanayotokea huku Tanzania. Kwa kifupi, mambo yameharibika. Natamani waraka wangu ungekufikia mwenyewe mkononi ili nikukumbushe ama nikupashe yanayoendelea huku.
Wale wote uliowanadi mwaka 1995 ili waienzi Ikulu yetu, walikugeuka miezi michache tu baada ya wewe kulala na babu zako. Wakaigeuza Ikulu kuwa sehemu ya biashara – ingawa wapo wengine uliwauliza “…Mnakimbilia Ikulu kufanya biashara gani!” Viwanda vyote ulivyopigania kuanzishwa waauziana wenyewe. Ikulu ikawa sehemu ya kusaini mikataba mibovu ambayo immeshuhudia madini yetu yalikuvunwa na kupelekwa nje huku sisi tukibaki na mashimo tu.
Kwa kifupi, uliona wanafaa walikusailiti. Maadili ya uongozi uliyoyasisitiza yakatoweka. Vita ya rushwa imeshindikana kwani wenye dhamana ya kupambana nayo ndio vinara wa kutoa na kupokea rushwa. Natamani hata Chifu Fundikira angekuwepo naye aone wenzake wanavyofaidi – pengine angesikitika kwa nini yeye aliondolewa kwenye Baraza lako la Mawaziri miaka michache tu baada ya uhuru.
Ufisadi umetamalaki kila kona, chaguzi zimegubikwa na rushwa mbaya. Chama chako cha Mapinduzi kimekuwa ‘Chama cha Matajiri’. Bora hili ni neon zuri, lakini wengine wanakiita ‘Chama cha Mafisadi’, au ‘Chama cha Majangili’ na wengine wanathubutu kusema ni ‘Chama cha Majambazi’, ilimradi kila mmoja anatamka neno analoona linafaa. Maskini hawana nafasi, wachache tu ndio wana sauti kwa sababu ya fedha zao.
Wale uliowapinga ndani ya Chama wakati ule, uliowahoji kuhusu walikopata utajiri wao, leo hii ndio wanaoabudiwa. Mbaya zaidi wanapita mpaka misikitini na makanisani kutoa misaada, halafu wanapigiwa makofi na kuimbiwa mapambio. Ungewaona, nina imani ungemwaga machozi. Naamini mama yetu Maria anaugulia moyoni kwa yanayotokea.
Mwalimu, sikuwepo wakati huo, lakini nakumbuka ilikuwa Jumapili, Aprili 26, 1964, saa 4.00 asubuhi wakati wewe – ukiwa Mwenyekiti wa TANU – ulipokutana na Mwenyekiti wa Afro-Shiraz Party (ASP) Sheikh Abeid Amani Karume mjini Dar es Salaam na kusaini hati ya makubaliano ya kuziunganisha nchi zenu. Muungano huu ulifikiriwa kwa takribani miezi mitatu na siku 24 tu tangu yalipofanyika mapinduzi ya kuung’oa utawala dhalimu wa Kisultani visiwani Zanzibar Januari 12, 1964. Kabla ya kutiwa saini, nyote wawili mlikuwa mmefanya mazungumzo mara kadhaa mjini Dar es Salaam na Unguja na ndipo mkafikia mwafaka wa kuziunganisha nchi hizo.
Wapo walioupinga wakati huo (na wanaendelea kuupinga) kwamba haukufuata misingi inayotakiwa katika muungano halisi, lakini pia wapo walioufurahia na wanaendelea kuufurahia kwa kuwa umeleta udugu na kujenga umoja na mshikamano.
Mwalimu, imebaki miezi michache tu ili Muungano huu utimize miaka 50, lakini nina mashaka kama hautakufa kabla ya miaka hiyo kutimia. Umoja, amani, upendo na mshikamano uliojengwa na muungano huo umetoweka kabisa.

Mapato yalikuwa makubwa, lakini wakaubinafsisha Mradi

 

 

HUU ni mfululizo wa Ripoti Maalum kuhusiana na mgogoro wa ardhi Kapunga wilayani Mbarali, mkoani Mbeya kama unavyoendelea kusimuliwa na Mwandishi Wetu DANIEL MBEGA, ambaye aliyefanya uchunguzi kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu. Endelea na Sehemu hii ya Saba…

 

MRADI uliokuwa unategemewa kuwa mkombozi wa Taifa katika suala la uzalishaji wa chakula, Continue reading “Mapato yalikuwa makubwa, lakini wakaubinafsisha Mradi”

Harakati za Chifu Mkwawa baada ya ushindi wa Lugalo

RIPOTI MAALUM CHIFU MKWAWA (7):

 

HUU ni mfululizo wa Makala ya Uchunguzi kuhusiana na historia ya kiongozi mkuu wa Wahehe, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Kilonge Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, kama yanavyoandikwa na Mwandishi Wetu DANIEL MBEGA, ambaye amefanya uchunguzi kwa takriban miezi mitatu sasa katika kuhimiza utalii wa ndani na kuhifadhi historia yetu. Endelea na Sehemu hii ya Saba…

 

BAADA ya ushindi wa Lugalo, Chifu Mkwawa hakutulia, bali aliendelea kuimarisha himaya yake pamoja na jeshi lake. Continue reading “Harakati za Chifu Mkwawa baada ya ushindi wa Lugalo”

Tusipoangalia tutaibinafsisha Serikali

Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye utawala wake ndio unaotajwa kutekeleza ‘kwa vitendo’ sera ya ubinafsishaji.

 

Na Daniel Mbega

 

BADO najiuliza bila kupata jibu sahihi kuhusiana na Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ya mwaka 1992 ambayo ilishuhudia mabadiliko katika mashirika 400 yaliyogawanywa katika makundi matatu makuu – mashirika Continue reading “Tusipoangalia tutaibinafsisha Serikali”

Biashara ilivyofuta Utakatifu Ikulu

 

 

Na Daniel Mbega

 

SIYO siri kwamba, viongozi wetu wa sasa wa Serikali wamechafuka, wameoza na kuvunda kutokana na kukosa uadilifu na uaminifu. Rushwa imetamalaki kila kona, wengi wametumia na wanaendelea kutumia vyeo vyao, ambavyo ni dhamana, kujilimbikizia mali.

Jinsi wanavyopigana vikumbo kila mahali kuusaka uongozi ni dalili pekee kwamba, Continue reading “Biashara ilivyofuta Utakatifu Ikulu”

Von Zelewiski auawa kwa kupigwa nyundo

HUU ni mfululizo wa Makala ya Uchunguzi kuhusiana na historia ya kiongozi mkuu wa Wahehe, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Kilonge Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, kama yanavyoandikwa na Mwandishi Wetu DANIEL MBEGA, ambaye amefanya uchunguzi kwa takriban miezi mitatu sasa katika kuhimiza utalii wa ndani na kuhifadhi historia yetu. Endelea na Sehemu hii ya Sita…

 

HADI wakati huo, tayari von Heydebreck – mmoja wa manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na kuanguka akiwa amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake: “…Mfululizo wa matukio hadi wakati huu ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua hilo kabla ya kujeruhiwa, Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma vichakani baada ya kufyatua risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi cha Tano tulilazimika kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija katika umbali wa hatua 30. Kama sikosei, Continue reading “Von Zelewiski auawa kwa kupigwa nyundo”