Home > All Stories > Kilimo na Mazingira kwa ulimwengu wa kijani

Kilimo na Mazingira kwa ulimwengu wa kijani

Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Tangu zamani sekta hiyo imetoa mchango mkubwa katika pato la Taifa kupitia mazao ya biashara kama Karafuu, Pamba, Katani, Kahawa, Chai na kadhalika. Lakini pia mazao ya chakula kama Mahindi, Mtama, Viazi Vitamu na kadhalika yamewanufaisha wananchi kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza kipato.

Hata hivyo, kutokana na mabadiliko makubwa ya mazingira, kilimo kimeonekana kupoteza mwelekeo ambapo ardhi imegugumia, watu wameamua kulima kwa kuhamahama kama wafugaji na hili limesababisha migogoro mikubwa baina ya jamii za wakulima na wafugaji. Wakulima wamevamia hata maeneo tengefu kwa ajili ya kutafuta ardhi yenye rutuba.

Matumizi ya mbolea za kemikali nayo yamesababisha ardhi kuzeeka haraka kwa kuzalisha sumu ambayo haiwezi kuondoka kirahisi. Pamoja na mbolea hizo, lakini si wananchi wote wanaoweza kupata ruzuku ya mbolea na pembejeo nyingine, hali ambayo imefanya kuwepo na uharibifu wa mazingira na pia kipato cha kaya kupungua.

Sote kwa pamoja tunaweza kusimama na kutetea uharibifu wa mazingira, lakini kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu kilimo hai kwa kutumia mbolea za mboji mboji badala ya kemikali. Hii nitasaidia wakulima waendelee kutumia maeneo yao yale yale ya siku zote bila kuhamahama na hivyo kuepusha ukataji ovyo wa misitu, vitendo ambavyo vinaharibu pia makazi ya wanyamapori na hivyo kuathiri sekta ya utalii.

Serikali na taasisi zote – za umma na binafsi – zinapaswa kushirikiana kwa karibu kuhakikisha Kilimo Hai kinahubiriwa kila kona kwa sababu kitawasaidia hata wakulima wetu kwa vile bidhaa za kilimo hai zina soko kubwa kimataifa.

Karibuni sana.

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: