Home > All Stories > Soko la SIDO Mbeya laungua

Soko la SIDO Mbeya laungua

“Kweli utu umekwisha na kilichobakia sasa ni unyama. Tazama wanavyosomba vitu kwenye duka langu na kutokomea navyo. Nakimbia moto, lakini watu hawa wanaojifanya wasamaria badala ya kunisaidia kunusuru mali yangu wao wameamua kuchukua vyote,” anasema Bi. Sitikege, kama alivyojitambulisha kwa jina moja, huku akiwa amechanganyikiwa.

Na lazima achanganyikiwe kwa sababu katika majira haya ya saa 4:30 leo hii, wafanyabiashara wote katika soko la SIDO Mwanjelwa, jijini Mbeya walikuwa wamechanganyikiwa kufuatia moto uliozuka na kuteketeza sehemu kubwa ya soko hilo, huku wengi wao wakipoteza mali nyingi ama kwa kuteketea kwa moto au kwa kuporwa na watu waliojifanya wasamaria wema.

Bi Sitikege, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wa soko hili, akiwa anauza vifaa vya elekitroniki kama redio na antenna za luninga kwenye duka lililoandikwa SIMSUNG, aliendelea kulalama bila kuwa tayari kupigwa picha; “Nimepoteza kila kitu, watu wamevamia duka langu, badala ya kuokoa mali wameamua kujisombea vitu vyote duka limebaki jeupe.”

Mama huyo ambaye alionekana kushikwa na fadhaa, alishindwa kuuzuia umati wa ‘wasamaria wema’ waliovamia dukani kwake mara baada ya jengo moja ambalo lina mashine za kukamulia mafuta ya alizeti kushika moto ambayo iliteketeza sehemu kubwa ya katikati ya soko hilo.

Soko hilo lilijengwa na manispaa kama mbadala kufuatia kuungua kwa soko la Mwanjelwa Desemba 2006 ambalo bado linaendelea kujengwa, na kwa kiasi kikubwa, soko hili la muda limekuwa ndilo kiini cha uchumi wa jiji la Mbeya.

“Tunashindwa kuelewa nini chanzo, ingawa wanasema kulikuwa na hitilafu ya umeme. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba, hivi kweli hatuna uwezo wa kukabiliana na majanga kama haya ama tunasubiri yatokee ndipo tuanze kuhangaika? Kwa nini tuna kawaida ya kukonyeza gizani?” alihoji Bwana Rashid Sanga, mmoja wa wananchi waliofika kwenye eneo la tukio kutoa msaada.

Moto huo ulianza saa 9:30 asubuhi na chanzo chake kinadaiwa kuwa ni shoti ya umeme iliyoanzia katika mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti na kuanza kusambaa katika fremu za maduka mengine.

Mali za mamilioni ya fedha zinadaiwa kutekea kwa moto na nyingi kuhamishwa na ‘wasamaria wema’ ambao mara nyingi huombea majanga kama hayo yawapate wenzao ndipo nao wajipatie mali kwa njia ya wizi.

Hii ndiyo hali halisi iliyokuwepo kwenye tukio hilo kama nilivyoishuhudia mwenyewe;

Moto ukiwa umeanza kupamba moto katika soko la SIDO, Mwanjelwa jijini Mbeya leo hii.

Moto unavyozidi kupamba kwenye soko la SIDO, Mwanjelwa leo asubuhi

Hali ni tete, moto unazidi kukolea katika soko hili la SIDO Mwanjelwa.

Ndiyo hali halisi ya namna moto ulivyokuwa hapa

Gari la Zimamoto likiwa limefika na kuanza kusaidia kuzima

Hali si shwari, wafanyabiasha wanaanza kujihami kwa kuondoa bidhaa zao

Kama kawaida yetu, maji yamekwisha na moto unazidi kukolea. Nani afanye nini?

Tufanyeje sasa, ndivyo wananchi wanavyojiuliza huku wakishuhudia moto ukipamba. PICHA ZOTE NA DANIEL MBEGA.

Wananchi 'wakisaidia' kutoa bidhaa ndani ya maduka

'Wasamaria wema' wakibeba kila walichokiona ndani ya maduka huku wafanyabiashara wakiwa wanaangua vilio

'Wasamaria wema' wamesaidia 'kuhamisha' mali ndani ya duka hili na kupeleka kusikojulikana

Si vibaya kuhamisha na ofisi

Advertisements
Categories: All Stories
  1. SHEMZIA MIRAJI SHEMBAGO
    November 11, 2011 at 2:18 pm

    Tunatakiwa wananchi wa mbeya kuwa makini na masoko yetu tuyajenge kwa matofari nasiyo mbao, hivyo jiji letu ni la ukweli hivyo tunatakiwa tuliendeleze zaid ili tuwe juu kama kawaida, ni mm mwanaharakati wenu SHEMZIA MIRAJI SHEMBAGO

  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: