Home > All Stories > Mbowe ataka wafanyabiashara Mbeya wafidiwe

Mbowe ataka wafanyabiashara Mbeya wafidiwe

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, wakitazama maafa yaliyotokea. (PICHA ZOTE NA DANIEL MBEGA).

Na Daniel Mbega, Mbeya

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameitaka Serikali kuwafidia wafanyabiashara wote waliounguliwa na mali zao kwenye Soko Kuu la SIDO jijini Mbeya juzi kwa kilichoelezwa kwamba ni uzembe mkubwa wa watumishi wa idara za serikali zinazohusika na uokoaji na kukabiliana na majanga.

Mbowe ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara katika eneo hilo wakati alipotembelea kujionea mwenyewe madhara makubwa yaliyosababishwa na moto huo.

“Huu ni uzembe wa serikali kushindwa kuudhibiti moto huu, na kwa hivyo wafanyabiashara wanapaswa kulipwa fidia na serikali. Tutasimamia na kuwapigania kuhakikisha mnafidiwa kwa sababu kama Zimamoto wangewahi na kuja kuifanya shughuli yao kwa makini, hakika yangeungua mabanda kama matatu tu na mengine yote yangeokolewa,” alisema Mbowe.

Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alisema kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vya uokoaji, moto huo ulipaswa kuzimwa ndani ya dakika 30 tu na si kutumia saa 5 ambazo hazikuzaa matunda.

“Kwa Marekani wanatumia dakika 10, Ulaya wanatumia dakika 15, na kwa nchini nyingine kama za Afrika, moto unatakiwa kuzimwa ndani ya nusu saa tu,” alisema.

Mbowe amewataka Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, na Mbunge wa Viti Maalum, Naomi Mwakyoma, kufuatilia kwa karibu kuhusu chanzo cha ajali, kuhakikisha wahusika wote wanashtakiwa na kufukuzwa kazi, kujua mali zilizoteketea za thamani gani pamoja na wafanyabaishara wangapi walioathirika, na mwisho kuona wafanyabiashara wote wanafidiwa,” alisema Mbowe.

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi, aliwataka wafanyabiashara wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki huku akiwaahidi kuwa nao bega kwa bega katika kufuatilia namna ambavyo wanaweza kufidiwa na serikali kwa kuwa huo ni uzembe wao.

Jumla ya vibanda 1,350 vilivyosajiliwa viliteketea vyote na kwa mujibu wa mashuhuda, madhara hayo ni makubwa sana kuliko yaliyolikumba Soko Kuu la Mwanjelwa mwaka 2006.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bi Beatha Swai, alisema serikali na vyombo vyote vinavyohusika, bado inaendelea kufanya uchunguzi na tathmini ya chanzo cha ajali hiyo pamoja na kujua uharibifu uliotokea.

“Hatuwezi kusema ni hasara kiasi gani iliyojitokeza, lakini tutawafahamisha baada ya vyombo husika kufanya uchunguzi wake,” alisema na kushindwa kueleza mikakati ya serikali kujihami na majanga ya aina hiyo huku akisema kwamba, suala la masoko liko chini ya Halmashauri na kwamba wao ni watawala tu.

Zifuatazo ni picha za matukio katika eneo hilo;

Mbowe akihutubia wananchi Jumamosi Septemba 17, 2011 kwenye eneo la soko la SIDO mjini Mbeya.

Umati wa wananchi wa Mbeya ukiomboleza mbele ya Mbowe

Hakuna anayejali moto. Watu wamevamia kwenye mabaki ya mabanda kutafuta chochote.

Akina mama nao wanachakura kwenye mabaki katika jengo la SIDO kuona kama wataambulia chochote cha maana.


Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: