Home > All Stories > Haya ndiyo maisha halisi ya kijijini

Haya ndiyo maisha halisi ya kijijini

Jamani eee, haya ndiyo maisha yetu halisi ya vijijini, tunakotokea wengi wetu ingawa tukiwa mjini huwa hatupendi kuyazungumzia kama ‘yanatuhusu’ wala kufanya juhudi za kuleta mabadiliko huko. Tukumbuke kwamba asilimia 83 ya Watanzania wako vijijini, sasa piga hesabu jinsi umaskini ulivyo huko. Tazama picha hizi ambazo zimepigwa na DANIEL MBEGA, Mod wa blogu hii.

Mojawapo ya nyumba nyingi za vijijini. Hapa ni katika kijiji cha Ilindi, wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Nyumba bora hii
Na hivi ndivyo vyoo vya ‘kisasa’

Boma la ng'ombe katika kijiji cha Ilindi

Jamaa ana kilo 110 akiwa hai. Wenyewe udenda unawatoka. Nilimkuta katika Kijiji cha Nghambi wilayani Mpwapwa hivi karibuni.

Mbegu bora kabisa ya Land Race. Ukifanya mchezo jamaa akitunzwa vizuri anaweza kufikisha hata kilo 250. Upo hapo?!

Mkubwa eeeh. Jonas Sajilo mkazi wa kijiji cha Nghambi wilayani Mpwapwa akimtazama nguruwe wa kaka yake, Mdajile, kabla ya kwenda kumchinja kwenye gulio la Kongwa.

Tunafuga kuku bora

Tunafuga pia nyuki kwa kutumia mizinga ya asili kama hii katika kijiji cha Ilindi, wilayani Bahi.

Lakini hata mizinga ya kisasa kama hii kutoka SIDO mkoani Dodoma imekuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wengi wa kijiji cha Ilindi. Medani Ibiga (35) akiwa na wanakikundi wenzake wa Kilimo Nyuki - Rose Sudayi na Ellen Sangula.

Ng'ombe hawa wa Medani Ibiga wametokana na ufugaji wa nyuki. Jamaa ana mizinga 175 ya nyuki na mwaka huu tu amevuna lita 281!

Wanaopenda ulabu jamani, hivi ndivyo komoni inavyopikwa mkoani Dodoma.

Ujamaa ni ushirika mkubwa kwa Wagogo iwe kiangazi au masika. Hapa wakazi hawa wa Nghambi wakimenya karanga kwa ajili ya mbegu. Dodoma inasifika kwa kilimo cha karanga ingawa alizeti na ufuta ni mazao yanayokuja kasi kwa sasa.

Advertisements
Categories: All Stories
 1. Aidan Elieza
  February 16, 2012 at 1:23 pm

  Kazi nzuri!

 2. February 27, 2015 at 9:28 am

  Muleba”classic
  Vijijini Kuna majanga sana””pamoko sana wakazi wa muleba.

 1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: