Home > All Stories > Kikwete ateua Mkuu wa JKT

Kikwete ateua Mkuu wa JKT

RAIS wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amemteua Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba (pichani) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 14 Machi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya mkurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu jana ilisema kuwa Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba alizaliwa tarehe 22 Apr 1954 wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Meja Jenerali Ndomba aliandikishwa Jeshi mwaka 1976 na kutunukiwa kamisheni 1977.

Katika Utumishi wake amewahi kushika madaraka yafuatayo, Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi, Mkuu wa Wilaya Ngara, Mkuu wa Mkoa Arusha na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi.

Meja Jenerali Ndomba anashika nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Samweli Kitundu ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: