Home > All Stories > Mattaka asomewa mashtaka sita mapya

Mattaka asomewa mashtaka sita mapya

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemsomea mashtaka mapya sita Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake.

Mashtaka hayo yanahusu matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Dola 143,442.75 za Marekani na zaidi ya Sh200 milioni za Tanzania.

Kabla ya kusomewa mashtaka hayo mapya, Mattaka na wenzake walishtakiwa kusomewa maelezo ya awali yanayohusu mashtaka matatu yaliyokuwa yakiwakabili.

Maelezo hayo yalihusu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kununua magari ya mitumba kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004.

Akiwasoma hati mpya ya mashtaka jana  mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo, Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro alidai kati ya Machi na Julai mwaka 2007 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Mattaka,  Elisaph Ikomba na William Haji wakiwa wa ATCL na wenzao ambao hawajulikani  walikula njama ya matumizi mabaya ya madaraka.

Alidai kuwa kitendo hicho kinapingana na  kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007.

Kimaro alidai kuwa  kati ya Juni na Julai mwaka 2007 washtakiwa walitumia vibaya madaraka yao kwa kutangaza zabuni ya ununuzi wa magari 26 yaliyochakaa, kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu cha 21 cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004.

Wakili huyo wa Serikali pia alidai kuwa washtakiwa wakiwa waajiriwa wa ATCL pia waliyatumia vibaya madaraka yao kwa kuagiza  magari 26 chakavu kwa gharama ya Dola 809,300 za Marekani kutoka Kampuni ya Bin Dalmouk Motors ya Dubai bila  kutangaza zabuni ya ushindani,  kitendo ambacho kilikiuka  kifungu cha 59 cha sheria ya manunuzi ya umma.

Pia alidai kuwa  washtakiwa  kati ya Julai na Agosti mwaka 2007 wakiwa jijini Dar es Salaam, washtakiwa walitumia vibaya madaraka yao kwa kununua magari hayo kwa niaba ya ATCL.

Mwendesha mashtaka pia alidai kuwa   kati ya Julai 2  na Agosti 23 mwaka  2007  katika Wilaya ya Ilala kwa nia ya kutenda ovu, washtakiwa  waliruhusu kununuliwa kwa magari hayo kutoka Dubai  bila ya kuwapo kwa mkataba  wa manunuzi ambao umewekwa saini na wahusika na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wakili Kimaro  alidai kuwa  kati ya Julai 2007 na Desemba mwaka 2011, jijini Dar es Salaam washtakiwa  walishindwa kuchukua tahadhari  kwa  kununua magari 26 chakavu toka Kampuni ya Bin Dalmouk Motors bila ya kuwapo kwa bajeti  ambayo ililenga manunuzi hayo na kuisababishia Serikali hasara ya Dola  143,442.75 za Marekani  baada ya Serikali kushindwa kuyalipia kodi  na kuchukua mkopo  kwa ajili ya kuyakomboa na kuyatunza.

Hata hivyo, washtakiwa walikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi umekamilika na kuomba kuwasomea maelezo ya awali.

Mattaka anayetetewa na wakili Peter Swai na Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Elisaph Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji anayetetewa na wakili Alex Mgongolwa waliomba wapewe muda wa kuyapitia maelezo hayo.

Hakimu Tarimo alikubaliana na ombi hilo na kutoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa hao ikiwa ni pamoja na  kutoa fedha taslimu Sh38.251 milioni  au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

 

Tembelea hapa:

http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/21181-mattaka-asomewa-mashtaka-sita-mapya

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: