Home > All Stories > Mtihani sasa kusahihishwa kwa mashine

Mtihani sasa kusahihishwa kwa mashine

 

BARAZA la Mtihani la Tanzania (Necta), limetangaza kuanza kutumia mashine maalumu katika usahihishaji wa mtihani wa taifa wa darasa la saba utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Taarifa ya Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, ilisema, teknolojia hiyo ‘Optical Mark Reader’ (OMR), itaanza kutumika katika mtihani wa majaribio kwa wanafunzi wa darasa la saba utakaofanyika Juni mwaka huu.

Ilisema kwa msingi huo, walimu wakuu wa shule za msingi kote nchini wanapaswa kuhakikisha kuwa wanafunzi wa  darasa la saba wanaanza kutumia fomu za OMR katika mtihani wa Juni, ili kupata uzoefu katika kuzitumia kwenye mtihani wa taifa.

Taarifa hiyo ilisema kutakuwa na karatasi maalumu kwa ajili ya kujibia maswali  ya mtihani ambayo baadaye, itasahihishwa kwa kutumia mashine.

“Teknolojia hii itaongeza kasi ya usahihishaji wa mtihani na hivyo kuliwezesha baraza kutoa matokeo ya mtihani mapema zaidi. Itapunguza sana muda mwingi uliokuwa ukitumika kuhakiki usahihishaji wa mitihani,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema hatua hiyo pia itasaidia kurahisisha uchambuzi  wa maswali ya mtihani kwa sababu matumizi ya mashine yataonyesha maswali yaliyojibiwa vizuri na yale yenye changamoto na  hivyo kuwapa nafasi wadau wa elimu kuchukua hatua stahiki.

Taarifa lisema,teknolojia pia itapunguza gharama za usahihishaji wa mitihani hasa ikizingatiwa kuwa ni wafanyakazi wachache tu watakaohitajika kufanya kazi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, huko nyum kazi ya kusahihisha mitihani ilikuwa inafanywa na watahini wapatao 4,000.

“Vyuo vya ualimu sasa vitakuwa na fursa ya kuendelea na kazi ya ufundishaji wa wanachuo maana vyuo  havitatumika tena  kwa kazi ya usahihishaji  wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi,” ilisema taarifa hiyo.

 

Source: Mwananchi

http://www.mwananchi.co.tz/biashara/13-biashara-za-kitaifa/21176-mtihani-sasa-kusahihishwa-kwa-mashine

 

 

 

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: