Home > All Stories > Takukuru: Mahakama ya K’ndoni yakithiri rushwa

Takukuru: Mahakama ya K’ndoni yakithiri rushwa

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema kuwa Idara ya Mahakama katika Mkoa wa Kinondoni imekithiri kwa rushwa na kusababisha  baadhi ya wananchi kukosa imani na Serikali yao.

Taasisi hiyo imetaja utolewaji wa nakala za hukumu na  dhamana kuwa ni kati ya mambo yaliyoongoza kulalamikiwa na wananchi katika mkoa huo.

Akizungumza  na watumishi wa Idara ya Mahakama Mkoa wa Kinondoni, Mkuu wa Dawati la Elimu Kwa Umma Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Mariam Mwendamseke  alisema kuwa mwaka 2011/012 zilitolewa taarifa 14 kuhusu malalamiko hayo ambapo walifanikiwa kufungua kesi tatu huku nyingine  zikiendelea kuchunguzwa.

Alisema kati ya mwaka 2009/010 zilitolewa taarifa saba ambapo kesi moja ilifunguliwa na mwaka 2010/2011 zilitolewa taarifa nne na kwamba nyingine  zilishauriwa kiutawala.

“Mmomonyoko wa maadili na ubinafsi wa baadhi ya watumishi wa umma ndiyo umekuwa chanzo cha rushwa,”alisema Mwendamseke.

Hata hivyo Afisa Masijala Mkuu katika Mahakama ya Kinondoni, Ngasala Sokolo alijitetea kuwa uhaba wa watumishi hasa katika uchapaji wa nakala  za hukumu umesababisha nakala hizo kuchelewa kutolewa na kupelekea malalamiko.

“Wilaya yetu tuna mahakama tano za mwanzo na zote hizo hazina wachapaji nakala zao zinachapwa hapa wilayani ambako nako kuna wachapaji wawili  tu,”alisema Sokolo na kuongeza:

“Hawana uwezo wa kutoa nakala 100 kwa siku moja, umeme nao ni tatizo tunaweza kukaa hadi  tatu bila umeme,”alisema.

Alisema watumishi wengi wa ngazi za chini wamesahaulika hasa katika ngazi za mishahara na kwamba hawapewi posho kama Mahakama za Rufaa, Biashara  na Ardhi.

“Sisi tumekuwa kama watoto yatima, wenzetu hadi chai wanayo tena ya maziwa na posho wanalipwa kati ya Sh150,000 hadi 200,000 lakini, sisi huku  hata hiyo Sh50,000 hakuna hali hiyo inatusononesha sana,”alisema.

Hakimu Mkazi Ferdinand Kiwonde alisema kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei kumesababisha watumishi wengi kuwa na hali ngumu  kwani hawana posho za usafiri wala nyumba.

Naye Mwanasheria wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni Joseph Kiula alisema kukosekana kwa mpangilio mzuri wa posho katika utumishi wa  umma kumesababisha kuwapo kwa malalamiko kwa baadhi ya watumishi na kwamba ugumu wa maisha nao unaweza kuwashawishi watu kuingia katika masuala ya rushwa.

 

Isome zaidi hapa:

http://www.mwananchi.co.tz/biashara/-/21177-takukuru-mahakama-ya-kndoni-yakithiri-rushwa

 

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: