Home > All Stories > Umeme wa upepo kugharimu dola mil. 136

Umeme wa upepo kugharimu dola mil. 136

KAMPUNI ya Power Pool East Africa Ltd (CDIG) ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kutumia dola milioni 136 za Marekani katika ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme wa upepo wilayani Singida.

Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Machwa Kagoswe, alisema hayo juzi wakati alipozungumza na Tanzania Daima katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme wa upepo lililoko kijiji cha Kisasida.

Alisema kati ya fedha hizo, dola 85 milioni zitatokana na mikopo mbalimbali na zingine 15, zitatolewa na wabia.

Kagoswe alisema ujenzi wa mradi huo mkubwa utaanza Julai mwaka huu na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi 18.

“Tunatarajia kati ya Januari na Machi mwakani tuanze kuzalisha megawati kati ya 10 na 30 kwa ajili ya kuziingiza kwenye gridi ya taifa,” alisema.

Aidha ofisa huyo alisema wanatarajia mwakani mradi utaanza kuzalisha megawati 50 kwa kuanzia na kwamba kila mwaka utakuwa unaongeza megawati 50 na itakapofikia mwaka 2015 mradi utakuwa unazalisha megawati 150 na kuziingiza kwenye gridi ya kitaifa.

Kasogwe alisema licha ya mradi huo kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa umeme, pia utapunguza uhaba wa ajira mbalimbali kwa sababu unatarajiwa kuajiri Watanzania wengi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, alimhakikishia Rais Zheng Xiangzhi, wa kampuni ya China Dalian International Economic and Technical Cooperation Group Ci.Ltd. inayojenga mradi huo kuwa serikali ya mkoa itakuwa bega kwa bega kuhakikisha shughuli za mradi huo hazikwami.

Alisema mkoa una wajibu wa kufanya hivyo kwa sababu mradi huo ni mkubwa kitaifa na ni kipaumbele cha serikali kuu, kwa kuwa unatarajiwa kupunguza kwa asilimia kubwa uhaba wa umeme nchini.

Naye rais Zheng, aliiahidi serikali ya mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa kama ratiba yake inavyosema.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: