Home > All Stories > Wakamatwa na meno tembo ya Sh6 mil

Wakamatwa na meno tembo ya Sh6 mil

POLISI mkoani Ruvuma inawashikilia watu wanne wakazi wa Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukutwa na vipande 80 vya meno ya Tembo, yenye uzito wa kilo 71.3 yenye thamani ya Sh6.4 milioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo lilitokea jana (Machi 15, 2011) saa 1:30 usiku neo la Mashamba ya Nafco, Kijiji cha Suluti, wilayani Namtumbo.

Kamuhanda alisema askari wa doria waliwakamata watu wanne wakiwa wamebeba vipande vya meneo ya tembo, ambayo yalikuwa yamepakiwa katika gari iliyokuwa imebandikwa namba za bandia DFP 7208 aina ya Toyota Land Cruise, mali ya mkazi wa Dar es Salaam.

Alisema uchunguzi uliofanywa na polisi umebaini meno hayo yalikuwa yakisafirishwa kutoka Namtumbo kwenda Dar es Salaam.

Alisema hilo ni tukio la kwanza tangu mwaka huu kuanza na alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kuwabaini watuhumiwa wanaojihusisha na biashara hiyo, ili kudhibiti uhalifu wa nyara za Serikali.

Kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Ujangiri Kanda ya Kusini, Omary Kitwara, alisema alipokea taarifa hizo kutoka kwa ofisa maliasili Wilaya ya Namtumbo na baadaye aliitwa na polisi kwenda kuthaminisha meno hayo.

Aliseman wanaweka mikakati madhubuti kukabiliana na majangili kwa kuwa, wana mbinu nyingi na soko lake kubwa ni China na Hong Kong.

Isome zaidi:

http://www.mwananchi.co.tz/biashara/13-biashara-za-kitaifa/21173-wakamatwa-na-meno-tembo-ya-sh6-mil

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: