Home > All Stories > Wakulima wa korosho wakataa stakabadhi

Wakulima wa korosho wakataa stakabadhi

BAADHI ya wakulima wa zao la korosho mkoani Lindi wameitaka serikali kuacha kuwalazimisha kuuza mazao kwa mpango wa stakabadhi gharani kwani mpango huo umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo yao.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa niaba ya wenzake kwa njia ya simu kutoka Kilwa jana, Ally Nananje, alisema haoni ulazima wa serikali kuwalazimisha kuuza mazao yao kwa kutumia mfumo huo ambao unawatia hasara.

Alisema wanalazimika kupinga mfumo huo kwa kuwa umekuwa ukiwatia hasara kutokana na bei zake kuwa za chini ukilinganisha na gharama za kilimo katika kuzalisha zao hilo.

Nananje alisema wanasikitishwa na utaratibu wa serikali kujitokeza wakati wa mavuno na kuwalazimisha wakulima hao wauze mazao yao kwa bei wanayotaka wakati haikusaidia chochote wakati wa kuandaa mashamba.

“Unajua serikali inatuonea, utakuta wakati tunahangaika kuandaa mashamba, kununua pembejeo na vitu vingine haionekani lakini tukishavuna ndiyo wanatujia tena mara nyingine hadi na polisi kututisha ili mradi tuiuzie mazao yetu kwa bei ya chini ambayo inatutia hasara; haya ni maonevu makubwa,” alilalamika Nananje.

Alisema serikali imekuwa ikiwalazimisha kuuza zao hilo la korosho kwa shilingi 1000 kwa kilo ambayo hailingani na gharama za kuandaa mashamba hadi wakati wa mavuno.

Nananje alisema serikali inapaswa kuwaacha wakulima hao wajichagulie ni wapi watauza mazao yao kwa bei yenye kuwaletea manufaa.

Alisema wapo wafanyabiashara ambao wako tayari kununua zao hilo kwa bei ya shilingi 1500 hadi 2000 kwa kilo bei ambayo ina maslahi kwao.

Nananje alisema iwapo serikali itaendelea kuwalazimisha kuuza mazao hayo kupitia mfumo huo wa stakabadhi gaharani itambue kuwa inajenga msingi wa umaskini wa kudumu kwa wananchi hao.

SOURCE: TANZANIA DAIMA

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: