Home > All Stories > Wakulima wa tumbaku wapata hasara ya mabilioni

Wakulima wa tumbaku wapata hasara ya mabilioni

 

Na Mwandishi Wetu
15th March 2012

Wakulima wa tumbaku wilayani hapa Mkoa wa Shinyanga,  wamepata hasara ya Sh. Bilioni 5.36 kwa msimu wa mavuno mwaka jana kwa kuyauzia makampuni zao hilo kwa bei ya chini.

Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo,  Deogratius Rugangila aliyasema hayo katika mkutano wake na wakulima wa vyama vya msingi vya Mweli na Itaganya vilivyopo Kata ya Bulungwa.

Rugangila alisema kwa upande wa wakulima wa kata hiyo,  wamepata hasara ya Sh. 1.3 sawa na 0.6 ya dola ya Marekani wanayolipwa na makampuni hayo ya ununuzi wa tumbaku.

Alisema kila soko lilikuwa likifanyika katika maeneo hayo, makampuni hayo yalikuwa yakikata kiasi cha Sh. 350,000 kwa ajili tumbaku ambayo ilikuwa inakutwa haina kiwango cha ununuzi.

Alisema hasara hiyo kubwa waliopata wakulima hao kwa kiasi kikubwa imetokana na kucheleweshwa kwa masoko kufanyika hali ambayo imewalazimu wakulima hao kuuza vshada vya tumbaku kwa walanguzi wanaonunua tumbaku vijijini.

‘Tatizo lenu wakulima wa tumbaku ni kuanza kuuza tumbaku yenu kabla hata hamjajua bei ya kununulia na kusababisha hadi kufikia hivi sasa wakati msimu umeisha mna tumbaku nyingine majumbani kwenu, ” alisema Rugangila.

Aliwataka wakulima kuwa makini katika kuuza tumbaku yao kwa makampuni ya ununuzi kwa kuwa yamekuwa na urasimu mkubwa kwao hivyo kuzidi kuwa maskini badala ya kunufaika.

Kuhusu malipo ya awali waliyokuwa wakiyadai Makampuni hayo, walisema  yamelipwa na kwamba hakuna mkulima anayedai.

Mkutano huo baina ya vyama hivyo ulifanyika kufuatia wakulima wa zao hilo kushutumu Afisa huyo mbele Mbunge wa Kahama, James Lembeli katika mkutano wa hadahara uliofanyikakatika kata hiyo kuwa amekuwa akichangia wasilipwe vizuri.
CHANZO: NIPASHE

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: