Home > All Stories > Polisi wakamata mirungi ya mil.15/-

Polisi wakamata mirungi ya mil.15/-

POLISI mkoani Arusha wamekamata dawa za kulevya aina ya mirungi zikiingizwa kutoka nchini Kenya kupitia Mkoa wa Arusha yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 15.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Arusha, Thobiasa Andengenye amesema jana kuwa, mirungi hiyo ilikamatwa saa moja na nusu jioni katika eneo la Lengijave, kijiji cha Elikoroti wilayani Arumeru ikiwa kwenye gari aina ya Canter lenye namba T 306 BUN.

Alisema, kukamatwa kwa dawa hizo kulitokana na taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilizoisaidia Polisi kuweka mtego ambapo polisi mwenye sare alijaribu kulisimamisha lakini halikusimama.

Alifafanua kuwa, baada ya gari hilo kugoma kusisimama askari waliamua kufyatua risasi moja hewani kwa lengo la kulisimamisha lakini halikusimama ndipo askari hao kwa kutumia gari lao la kawaida walilifukuza na kulipiga risasi tairi ya nyuma likasimama.

Kamanda Andengenye alisema baadhi ya wahusika wa gari hilo akiwemo dereva wa gari hilo ambaye hakufahamika, walifanikiwa kukimbia na kulitelekeza.

Alisema kuwa Polisi inamshikilia mtuhumiwa mmoja Emanuel Olemejooli (19), mkazi wa Engikaret anayedaiwa kufanya kazi ya kuvusha magari yanayosafirisha dawa za kulevya.

Aliongeza kuwa dawa hizo ni viroba 95 vya mirungi vyenye uzito wa kilogramu 3,000 na thamani yake ni zaidi ya milioni 15 na kwamba viroba hivyo vilikuwa na majina mambalimbali huku baadhi yake vikisafirishwa kwenda mikoa ya Singida, Mwanza, Tabora, Manyara, Shinyanga na Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Mkoa wa Arusha, Hamis Warrioba alisema kuwa wafanyabiashara wa dawa hizo wana mtandao mkubwa kwa kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa wa hapa nchini na wengine kutoka Kenya.

Alisema, kitengo chake kimejizatiti kukabiliana na biashara hiyo haramu kwa kuweka doria sehemu zote zikiwemo njia za panya ambako magari yanayovusha bidhaa hiyo yamekuwa yakipita na kinatarajia kuteketeza dawa hizo kesho baada ya Mahakama kujiridhisha.

Katika hatua nyingine SP Warioba alidai kuwa Polisi imekuwa na wakati mgumu kuvishinda vishawishi kwani muda mfupi mara baada ya kukamata dawa hizo baadhi ya wafanyabiashara walijitokeza kujaribu kutaka kuwahonga Sh milioni 10 ili waliachie gari hilo, lakini walikataa na kulifikisha Kituo cha Polisi.

CHANZO; HABARILEO

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: