Home > All Stories > Maryanne Tutuma ndani ya Pasaka

Maryanne Tutuma ndani ya Pasaka


Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI wa muziki wa Injili kutoka Kenya, Maryanne Naipasoi Tutuma amethibitisha kushiriki tamasha la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, alisema Maryanne amekubali kushiriki.

Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu atatua nchini akiwa na albamu yake ya Ilmaasae Asai aliyoiimba kwa lugha ya Maasai.

Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

Aliongeza kwamba Maryanne atakuja nchini na waimbaji wake na ataimba ‘live’ siku hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu lina malengo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wajane wasiojiweza.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Mbali na Maryanne, wasanii wengine wa nyimbo za Injili watakaopamba tamasha hilo ni Rebecca Malope, Rose Muhando, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka na Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka DRC.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia.

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: