Home > All Stories > Asilimia 36.5 Tanga waishi katika umaskini wa kutisha

Asilimia 36.5 Tanga waishi katika umaskini wa kutisha

ASILIMIA 36.5 ya wakazi wa Mkoa wa Tanga, wamedaiwa kuishi kwenye umaskini wa kutisha huku wengi wao wakidaiwa kushindwa kukidhi mahitaji muhimu ya kibinadamu kama chakula, malazi na mavazi.
Hayo yamo katika Rasimu ya Mpango wa Uwiano wa Maendeleo wa Mkoa wa Tanga. Kwa mantiki hiyo, hali hiyo duni imepelekea wananchi wengi kushindwa kuchangia huduma za kijamii kama Afya, Maji na Elimu.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo, Changamoto hizo zimethibitishwa katika matamshi na maandishi kutoka kwenye mipango ya wilaya iliyoanisha kuwa, tatizo kubwa linalowakabili wananchi wa mkoa huu ni hali duni ya maisha.
Rasimu hiyo imetaja sababu mbalimbali zinazosababisha hali hiyo kuwa, ni pamoja na wakazi wengi kushindwa kupata milo mitatu iliyokamilika kwa siku (balance diet) huku hata wale waliofanikiwa kupata mlo huwa si kamili na wenye wingi wa wanga.
“Wakazi wengi hushindwa kusomesha watoto katika shule za sekondari na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na hivyo vijana wengi huishia kwenye kiwango cha elimu ya msingi,” imefahamika kutoka rasimu hiyo
Hata hivyo rasimu hiyo imeeleza kuwa umaskini wa kipato unatokana na uzalishaji duni wa mazao ya kilimo na mifugo, hasa ikizingatiwa kuwa asilimia 80 ya wakazi wa Tanga ni wakulima na wafugaji.
Hali hii pia imechangiwa na kufa kwa viwanda vingi kutoka viwanda 108 mwaka(1990) hadi viwanda 55 mwaka(2010), ambavyo vilikuwa vinatoa ajira kwa idadi kubwa ya wakazi wa mkoa huu.
Pia imeelezwa ufugaji usio na tija kwani wakazi wengine bado wanafuga kienyeji, mfano ng’ombe wa maziwa wa Handeni, Mkinga na Kilindi anatoa lita7 badala ya lita 10-15 kwa siku.
Rasimu hiyo imeelezwa kuwa kwa kuwa mpango huu ni wa maendeleo ya wananchi wa Tanga, basi hakuna budi suluhu ya matatizo hayo yakaanza kutafutiwa ufumbuzi wa hali halisi ya watu wa mkoa huo na kutoa taswira iliyopo.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: