Home > All Stories > JK aapisha wakuu wa mikoa wapya

JK aapisha wakuu wa mikoa wapya

RAIS Jakaya Kikwete jana aliwaapisha wakuu wa mikoa minne wapya. Walioapishwa katika sherehe hizo ni pamoja na Dk Rajab Rutengwe ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Magalula Magalula anayeenda kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Wengine ni Paschal Mabiti ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu pamoja na Kapteni Asery Msangi aliyeapishwa kama Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Akizungumza baada ya kuapishwa, Mabiti alisema kuwa moja ya mambo atakayoyasimamia ni pamoja na suala zima la ulinzi na usalama, kusimamia shughuli za maendeleo na kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinafuatwa katika utekelezaji wa kila jambo.
Kwa upande wake Dk Rutengwe alisema kuwa uteuzi wake mkoani Katavi utamwezesha kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Pamoja na mambo mengine nitasimia sheria na kanuni zilizopo ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wangu,” alisema Dk Rutengwe
Katika hatua nyingine, Rais alivunja watu mbavu Ikulu baada ya kufanya utani wa hapa na pale. Rais alianza kumtania kwa staili ya aina yake Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli.
Kikwete alianza mzaha huo muda mfupi baada ya kuwaapisha na kupiga picha na wakuu hao wa mikoa mipya ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe.
Huku akiwa amezungukwa na Waziri mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, viongozi wa serikali, waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali , Rais Kikwete alimuita kwa sauti ya juu Waziri Magufuli, lakini akitumia jina  la Pombe ambalo pia ni jina la waziri huyo.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: