Home > All Stories > Maduka 11 ya kuuza dawa yafungwa Dar

Maduka 11 ya kuuza dawa yafungwa Dar

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Baraza la Famasia, limeyafunga maduka 11 yanayouza dawa za binadamu jijini Dar es Salaam kwa kushindwa kuweka wauzaji wenye taaluma ya madawa na kuuza dawa ambazo muda wake wa matumizi umeisha.
Naibu Msajili wa Balaza la Famasia, Leah Chenya, alisema katika msako ulioendeshwa jijini Dar es Salaam juzi, iligundulika kuwa baadhi ya dawa muda wake umeisha.
Alisema timu ya wakaguzi ilifanya ukaguzi katika maeneo ya Kimara, Mwananyamala, Sinza, Kijitonyama na kubaini makosa kadhaa ikiwemo wauzaji wa maduka hayo kutokuwa na sare, maduka ya dawa baridi kuuza dawa za moto na kutokuwa na vibali vilivyokamilika vya uendeshaji wa shughuli hizo.
“Tumewakuta wauzaji wasiokuwa na elimu ya madawa, wengi wao tuliokuwa tunawauliza walisema wanafanya kazi hiyo kwa uzoefu na hawajaenda shule kusomea,” alisema Chenya.
Mfamasia kutoka baraza hilo, Dominick Mfoi, alisema zoezi hilo litakuwa endelevu kwa kuwa serikali imepania kudhibiti utitiri wa maduka yanayoendelea kufunguliwa bila kufuata sheria.

CHANZO: NIPASHE

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: