Home > All Stories > Mamlaka za maji nchini zatakiwa kuboresha huduma

Mamlaka za maji nchini zatakiwa kuboresha huduma

WIZARA ya Maji imezitaka mamlaka za maji safi na majitaka nchini kuboresha huduma zake, ili zilingane na viwango vya kimataifa na kupata cheti cha utoaji huduma kwa kufuata taratibu za Kimataifa cha International Standard Organization (ISO 9001:2008).
Akikabidhi cheti cha utoaji huduma bora kimataifa (ISO) kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Moshi (Muwsa), Naibu Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, alisema zipo mamlaka 19 za maji safi na majitaka, lakini mpaka sasa ni tatu zilizopata cheti hicho.
Lwenge alizitaja kuwa ni Tanga, Arusha na Moshi na kwamba, kujisajili kutoa huduma kwa viwango vya kimataifa kutakuwa  kumekidhi mahitaji ambayo yamewekwa kwa viwango vya kimataifa.
Alisema Mausa imeonyesha ubora unaokubalika na tathmini ya utendaji inayofanywa na na Ewura kila mwaka imekuwa ikishika nafasi ya juu kati ya mamlaka 19 za miji mikuu ya mikoa nchini.
“Mamlaka hii imepata cheti cha ubora wa maji kutoka TBS kuanzia mwaka 2007 na kuendelea kuthibitishwa kila mwaka, cheti hicho kinaamanisha kwamba maji yetu yanakidhi viwango vya ubora wa maji Tanzania na Shirika la Afya Duniani (WHO),” alisema.
Alisema kwa Mkoa wa Kilimanjaro Muwsa imekuwa ikiongoza tangu mwaka 2002 kwa utoaji huduma na kwamba, imeweza kukusanya mapato ya wastani wa Sh3.6 bilioni kwa mwaka na kujiendesha yenyewe.
Awali, Mkurugenzi wa Mausa, Antony Kasonta, alisema mchakato wa kupata cheti cha ISO umechukua muda mrefu kwa kuwa ilijumuisha mambo mengi, ikiwamo kuundwa timu za ukaguzi wa ndani kuzipa mafunzo mbalimbali kufanya ukaguzi wa ndani na nje.
Alisema cheti cha ISO 9001:2008  kitawawezesha kufikia kwa urahisi malengo ya mpango mkakati ya mamlaka ya 2010/2015, kutoa huduma ya uhakika kwa majisafi na salama, kuboresha mfumo wa majitakana kuongeza uwezo wa mamlaka kujitegemea.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: