Home > All Stories > Meja Jenerali Kitundu apandishwa mahakamani

Meja Jenerali Kitundu apandishwa mahakamani

MEJA Jenerali wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Samwel Kitundu, ameburuzwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Kitengo cha Ardhi, akidaiwa kununua shamba la ukubwa wa ekari 20 lenye utata wa umiliki, lililopo Bamba, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wadaiwa wengine katika kesi namba 98 ya mwaka 2011 ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Stella Mugasha na Theobard Kibakaki, ambao wanashitakiwa na Silla Shekiondo na Petro Abdallah.
Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Jaji Lawrence Kaduri, wadai wanataka kurudishwa eneo lao hilo pamoja na kulipwa fidia ya sh milioni 300 kutokana na usumbufu wa kuvamiwa eneo lao.
Pia wanaiomba mahakama iamuru walipwe sh 200,000 kila mwezi tangu wadaiwa hao walipoanza kulimiliki isivyo halali shamba hilo pamoja na kulipa gharama za kesi.
Katika kesi hiyo, wadai hao wanaotetewa na Wakili Benjamin Mwakagamba wanadai kuwa Oktoba 5, mwaka jana, mmiliki wa shamba hilo, Cleophas Petro Katinda aliyefariki dunia Novemba 6, 2004 kabla ya kifo chake akiwa na akili timamu aliwapa idhini ya kumiliki shamba hilo na kwamba watagawana shamba hilo nusu kwa nusu kwa msaada wake (Katinda) na Steven Mtetemela wa Miko Constructions Co. Ltd.
Kutokana na hilo, wadai hao wanaeleza kuwa Meja Jenerali Kitundu alinunua shamba hilo isivyo halali kutoka kwa Kabakaki na Mugasha, kwani si sehemu za mali za marehemu Katinda.
Katika utetezi wao wa maandishi, wadaiwa hao wameeleza kuwa wamemuuzia kihalali eneo hilo Meja Jenerali Kitundu kwa sh milioni 10, hivyo kuiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo.
Wanadai kuwa katika uhai wake Katinda hajawahi kugawa eneo hilo, hivyo nyaraka zilizowasilishwa na wadaiwa hao ni za kughushi kwani hakuna nyaraka halisi zinazoonesha zilisainiwa na marehemu Katinda.
Kesi hiyo itatajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Mei 8, mwaka huu.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: