Home > All Stories > Rais afanya uteuzi wa Makatibu Tawala

Rais afanya uteuzi wa Makatibu Tawala

RAIS Jakaya Kikwete ameteua Makatibu Tawala wa Mikoa saba wakiwamo wanne wa Mikoa mipya na kufanya uhamisho wa wengine watatu.  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa,  Rais Kikwete amemteua Dk Faisal Hassan Haji ISSA, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro,Kabla ya hapo Dk Faisal alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Pia amemteua Mariam MTUNGUJA, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, ambaye awali alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.  Eliya NTANDU, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro. Kabla ya hapo Ntandu alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.
Vilevile taarifa hiyo imeeleza kuwa Severine Kahitwa, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Kabla ya hapo Kahitwa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dodoma.
Balozi Sefue katika taarifa yake hiyo alieleza kuwa Emmanuel Kalobelo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. Kabla ya hapo Kalobelo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasharui ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.   “Hassan Bendeyeko, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Kabla ya hapo alikuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro,”ameeleza taarifa hiyo.
Dk Anselem Tarimo, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya hapo  Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.  ‘Uteuzi huu unaanza rasmi tarehe 21 Machi, 2012 na wataapishwa Ikulu, Jumamosi  ya tarehe 24 achi, 2012 saa nne asubuhi.”
Waliohamishwa ni  Mgeni Baruani aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe. Mwingine ni Mwamvua Jilumbi aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa  Shinyanga anahamishiwa Mkoa wa Simiyu.  Bertha  Swai aliyekuwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya anahamishiwa Mkoa wa Pwani.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: