Home > All Stories > Ripoti ya maji Iringa yatisha

Ripoti ya maji Iringa yatisha

ZAIDI ya asilimia 75 ya maji yanayotumiwa na wakazi wa Iringa yamethibitika kuwa si salama baada ya Shirika la ACCRA la Njombe kufanya utafiti.
Meneja Mradi wa Shirika la ACCRA, Giorgio Colombo, alibainisha hayo jana wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo kwa wadau mbalimbali wa maji mkoani hapa katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika ukumbi wa Veta ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka, alikuwa mgeni rasmi.
Alieleza njia mbalimbali za kupima maji huku akizishauri mamlaka za maji mjini na vijijini kufanya utafiti, ili kubaini mahali sahihi ambapo maji yanachafuka kabla hayawafikia watumiaji.
Utafiti huo ulifanyika baada ya Sekretarieti ya Mkoa kwa kushirikiana na UNHABITAT na ACCRA ilipoandaa mafunzo Februari mwaka jana juu ya njia rahisi ya kupima ubora wa maji na kuyatibu.
Akifungua semina hiyo, Katibu Tawala huyo alizishauri mamlaka za serikali kuchukua jukumu la kuhakikisha watumiaji wa maji wanaunda vikundi vyao na maji yanayotumiwa na wakazi wa Mkoa wa Iringa yanapimwa.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: