Home > All Stories > Ufaransa yaifutia deni Tanzania

Ufaransa yaifutia deni Tanzania

NAIBU Waziri wa Fedha, Gregory Theu, ameishukuru Ufaransa kwa kuisamehe Tanzania deni la euro milioni 12.7 lililokopwa miaka 13 iliyopita na badala yake fedha hizo zinatarajiwa kutumiwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo maji safi na taka, elimu na utalii.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Shirika la AFD, yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa, Theu alisema kituo hicho kimewezesha Tanzania kunufaika kimaendeleo katika huduma ya kijamii kwa muda wa miaka 13.
Alisema kuwa kati ya maeneo yaliyonufaika na mradi huo nchini ni pamoja na Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo mradi wa maji umekamilika na utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wowote kuanzia sasa.
Alisema kuwa AFD ndio waliojenga Chuo cha Utalii ambacho ni rasilimali ya kutumainiwa itakayoendelea kuwepo kwa muda mrefu.
Hadi sasa AFD tayari wamefanya miradi mbalimbali katika nchi 80, ikiwamo Bara la Afrika, kusini mwa Mediterranean, mashariki mwa Bara la Asia zikiwemo nchi za India, Pakistan, China, Indonesia, Thailand, Latin America, Brazil, Colombia, Mexico na Thailand na nyinginezo nyingi.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: