Home > All Stories > Wakulima Karatu washauriwa

Wakulima Karatu washauriwa

WAKULIMA wilayani Karatu wameshauriwa kuchagua zao moja linaloendana na mazingira yao na kulima ili waweze kunufaika na kilimo hivyo kuondokana na umaskini.
Wito huo umutolewa na wadau mbalimbali  wa kilimo kutoka ndani na nje ya Wilaya ya Karatu katika mkutano wa siku moja  wa wadau wa kilimo uliojadili kuchagua zao moja lenye tija kwa kilimo wilayani humo.
Mkutano huo uliofunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Karatu Clement Berege ulihusisha maofisa mbalimbali wa kilimo na mifugo watakaotumika kuwaelimisha wakulima kuhusu ulimaji mazao yenye tija na manufaa kwao.
Katika mkutano huo ilipendekezwa kuwa mahindi yakilimwa kwa kufuata taratibu na kanuni za kilimo bora na wakulima wa Karatu litawaletea tija.
Zao hilo limependekezwa kuzingatia vigezo ambavyo ni pamoja na kuleta tija katika pato la halmashauri na mkulima, kuwa na soko la uhakika, kupatikana kwa pembejeo kwa urahisi pamoja na kuwa zao linalokubali mazingira.
Wadau hao pia waliunda kikosi kazi kitakachoandaa mpango unaofuata mnyororo wa thamani kwa zao lililochaguliwa wakishirikiana na Ofisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya ambapo kazi hiyo itatumwa Tamisemi baada ya kupitiwa na washauri wa kilimo wa Mkoa
Wakihitimisha Mkutano huo wadau hao wa kilimo na mifugo waliwashauri wakulima kote nchini kuacha kulima kilimo cha mazoea na kulima mazao yanastahimili mazingira na hali ya hewa katika mazingira husika ili waweze kunufaika na kilimo

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: