Home > All Stories > Walanguzi wa choroko wapigwa marufuku

Walanguzi wa choroko wapigwa marufuku

SERIKALI wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara imewapiga marufuku walanguzi wa zao choroko na imewataka wakulima wasidanganyike na badala yake wauze mazao yao kwenye vyama vya ushirika kwa mfumo wa stakabadhi ghalini.
Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Fatuma Alli alisema kuwa wanafanya jitihada ya kuwasaidia wakulima zao hilo baada ya msimu uliopita kudhulumiwa na walanguzi ambao walikuwa wakinunua kilo moja na robo ya choroko Sh300 na kutumia vipimo visivyo rasmi maarufu kangomba.
Agizo hilo alilitoa kwenye  mkutano wa watendaji, viongozi wa kimila na wananchi,  ulioofanyika tarafa ya Nakopi.
Alisema serikali imefanya jitihada za kukiamasisha Chama Kikuu cha Ushirika wilayani humo (Mamku) kununua zao hilo kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ili walikuma wasiendelee kuibiwa na wajanja ambao wananunua kwa kutumia vipimo visivyo rasmi na kwa bei ndogo.
Alisema Mamku kitakusanya choroko zote kwa wakulima kwa bei ya Sh800 na kuzipeleka kwenye maghala makuu na kwamba kutakuwa na mnada kwa wafanyabishara wanaohitaji kununua zao hilo.
Mkuu huyo wa wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliwaagiza watendaji vijiji na kata kuwajibika katika maeneo yao ili kuwathibiti walanguzi wa zao hilo.
Fatuma aliwataka watendaji wote kutojihusisha na walanguzi wa zao hilo na badala yake aliwataka wawafichue wanunuzi  hao.
“Ndugu zangu naamini walanguzi wote tuna watambua kwani ni miongoni mwetu, kama sio ndugu zetu basi wajomba zetu  hivyo ni vizuri sasa tukaamua kwenda kuwashauri waache  tabia hiyo ili kukomesha tatizo hilo,”alisema mkuu huyo.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: