Home > All Stories > Walimu kortini kwa tuhuma za mamilioni ya fedha

Walimu kortini kwa tuhuma za mamilioni ya fedha

WALIMU watatu wa Shule ya Msingi Tukoma, iliyopo Halmashauri ya Mpanda, mkoani Katavi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda pamoja na mzabuni wa halmashauri hiyo, wakikabiliwa na mashitaka 68 kwa tuhuma za wizi wa zaidi ya shilingi milioni ishirini na moja.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Kasele, washitakiwa hao ni Joel Mwakyusa ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Renatus Ngairo na Joachim Katabi, ambao ni walimu pamoja na Fredrick Mlenge, mzabuni wa Kampuni ya Royal Stationery.
Mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi Finias Majura, alidai mahakani hapo kuwa, washitakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Novemba 28, 2009 na Agosti 28 mwaka jana, kwa nyakati tofauti.
Miongoni mwa mashitaka 68 waliosomewa mahakamani hapo, ni pamoja na kula njama za kumuibia mwajiri wao wakiwa watumishi wa serikali, kumdanganya mwajiri wao na kujipatia kiasi hicho cha fedha.
Pia walidaiwa kutengeneza hati bandia ya kujipatia pesa kupitia Benki ya NMB, Tawi la Mpanda kwa kutumia jina la mwalimu mkuu wa Shule ya Tukoma kwa kutumia hundi namba 002490788 yenye thamani ya shilingi laki nane na nusu.
Mwendesha mashitaka, Majura alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao watatu ambao ni walimu ya Shule ya Msingi Tukoma kwa nyakati tofauti wakishirikiana na mzabuni wa Kampuni ya Royal Stationery walishirikiana kumuiba mwajiri ambaye ni Halmashari ya Wilaya ya Mpanda kiasi hicho cha fedha ambazo zilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule.
Washitakiwa hao wanne baada ya kusomewa mashitaka hayo, waliyakana. Walirudishwa rumande kwa kunyimwa dhamana na mahakama.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: