Home > All Stories > Madiwani wadai bajeti imejikita kwenye upendeleo

Madiwani wadai bajeti imejikita kwenye upendeleo

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, wameikosoa bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13 kwa madai kuwa haikuzingatia vipaumbele vilivyopitishwakwenye vikao vya kamati tendaji.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Eliya Mhecha, aliwasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2012/13, huku madiwani wakiomba wakuu wa idara na wataalamu kuzingatia vipaumbele badala ya kujipangia wanavyotaka wao wenyewe.

Diwani wa Kata ya Nyamisangora, Thobias Ghati (Chadema) na Diwani wa Kata ya  Kyore Kambarage (CCM), walisema kuna watu walifanyiwa tathmini ya ardhi, lakini kiwango cha fidia hakijabainishwa kwenye kabrasha la bajeti.

“Tuliazimia wananchi walipwe ardhi yao kama njia ya kusaidia vijiji vipate hati miliki na kupatiwa mikopo, tukachagua vijiji 30 vya kuanzia, lakini haijaingizwa kwenye bajeti kata yangu ya Kyore sijaona chochote siwezi kusema bajeti ipitishwe na wakati haya tuliyoazimia yameondolewa kwenye kabrasha,” alisema Kambarage.

Madiwani hao walisema moja ya vipaumbele vyao kwenye bajeti ya 20012/13 ni viporo ambavyo havikukamilika na kutekelezwa mwaka 2011/12.

“Kamati ya elimu, afya na maji tulikaa tukapitisha vipaumbele vyetu vitakavyowekwa kwenye kabrashahakuna, kila kamati inapaswa kusikilizwa vipaumbele vyake kuna kamati zingine zina mamlaka zaidi ya kamati zingine, kwanini Kamati ya Uchumi na Fedha ndiyo ichukue jukumu la kuondoa maazimio yetu na kujipangia wao wanavyotaka?” alihoji Mustapha Masiani, Diwani wa Nyarukoba (Chadema).

Kamati ya Uchumi na Fedha ilizidi kutupiwa lawama kwa madai kuwa ndiyo iliyohusika kutengua vipaumbele vilivyotolewa, huku wajumbe wa kamati ya elimu, afya na maji wakidai kuwa hawakutendewa haki baada ya kuondolewa vipaumbele vyao.

Diwani wa Kata ya Mbogi, Nyankomo Maganigwa (CCM), Diwani wa Kata ya Gorong’a, Magarya Omari (Chadema), Kata ya Pemba,Paradiso Sererya (CCM), Kata ya Binagi, Leonard Masyaga (Chadema) na Luis Thomas wa Kata ya Ganyange, walilalamikia  kutoingizwa kwenye mpango wa bajeti zahanati na shule ambazo hazijakamilika muda mrefu.

Diwani Kata ya Kibasuka, Seleman Moya (CCM), alisikitishwa bajeti hiyo kutowekwa fedha kwa ajili ya shughuli za mwanasheria wa halmashauri, ikiwamo fedha za kuwalipa makatibu wa mabaraza ya kisheria ya kata wanaofanya kazi bila malipo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri, Amosi Sagara, alishinikiza madiwani kupitisha bajeti hiyo kwa kile alichotetea kuwa, Serikali imekuwa ikitoa fedha kidogo.

Naye Mhecha alisema wameshindwa kuzingatia vipaumbele vyote kwa kile alichoeleza kuwa, Serikali zote za mitaa zinategemea ruzuku kuu ya Serikali ambayo haitoshelezi kila hitaji na kwamba, kuna haja ya kujikita kwenye vyanzo vya ndani vya mapaoto.

Halmashauri imeomba Sh30,583,564,242, kati ya hizo Sh5,102,685,800 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, Sh19,294,246,276 mshahara na Sh6,186,632,166 matumizi ya miradi ya maendeleo. Pia, halmashauri kupitia vyanzo vyake vya ndani inatarajia kukusanya Sh2,269,232,000.

Mapato halisi hadi kufikia Februari mwaka huu, halmashauri imepokea Sh14,445,294,496 na kwamba, matumizi halisi ni Sh4,227,361,381.

Hata hivyo, madiwani walisema fedha za mishahara zilizodaiwa kutumika kwa aslimia 100 ni uongo kwa madai kuwa, kuna watumishi walifukuzwa na wengine kusimamishwa kazi.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: