Home > All Stories > Ukarabati wa reli kuanza Mei 2012

Ukarabati wa reli kuanza Mei 2012

SERIKALI imesema kuwa iko mbioni kuanza kukarabati wa reli kwa kutandika reli ya uzito wa ratili 80 kwa yadi kutoka Kitaraka hadi Malongwe kuanzia Mei mwaka huu.

Imesema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 kutokana na ugumu wake ikieleza kuwa  baada ya kukamilika, mradi huo utaruhusu mawasiliano ya reli kwa njia hiyo hivyo kuweza kuinua pato la wananchi.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athman Mfutakamba alitoa kauli hiyo bungeni jana ambapo alisema kuwa Serikali itaendelea na mradi wa kuinua kiwango cha reli kutoka Kaliua na Mpanda kwa umbali wa kilomita 9 ikitumia mataruma yanye uzito wa ratili 56.5.

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Abdallah (CCM), aliyetaka kujua Serikali ina mikakati gani ya muda mfupi na mrefu wa ukarabati na ukarabati huo utaanza lini.
Mbunge huyo pia alitaka kujua kama Serika inaweza kuainisha ukarabati wa muda mrefu utakuwa hadi lini.

Akijibu swali hilo, Mfutakamba alisema kuwa Serikali itaendelea na mradi wa kuinua kiwango cha reli kutumia mataruma yenye uzito wa ratili 56.5 kwa yadi badala ya uzito wa ratili 45 kwa yadi.

“Kazi ya kuimarisha na kupanua tuta la reli kati ya Kaliua na Mpanda umbali wa kilometa 5 ilikamilika Machi, 2012,” alisema Mfutakamba.

Waziri huyo alitaja mipango mingine ya Serikali kuwa ni kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam hadi Isaka kwa kiwango cha kimataifa, ambayo itaunganishwa na reli mpya ya kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: