Home > All Stories > CAG achekelea vigogo wala rushwa kung’olewa

CAG achekelea vigogo wala rushwa kung’olewa

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ameeleza kufurahishwa kwake na namna ripoti yake ya mwaka uliopita wa fedha, ilivyopewa uzito na hatua kuchukuliwa dhidi ya wote waliotajwa kuhusika katika ubadhirifu wa rasilimali za umma.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Utuoh alimshukuru Spika wa Bunge, Anna Makinda, Bunge na Rais Jakaya Kikwete kwa namna walivyoipa uzito ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2010/11 na kuweza kujenga imani ya umma kwa Bunge na Serikali yake.

Hiyo ilitokana na matokeo ya mjadala wa ubadhirifu na ufisadi wa mabilioni ya shilingI uliotokea katika baadhi ya Wizara ambapo baada ya mjadala mkali bungeni, Rais Kikwete alilazimika kuunda upya baraza lake la mawaziri na kuwaacha nje baadhi ya mawaziri.

Mawaziri hao ni Mustafa Mkullo (Fedha), Cyril Chami (Viwanda na Biashara), William Ngeleja (Nishati na Madini), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii) na Omar Nundu (Miundombinu).

Katika kufungua mafunzo maalumu ya siku tatu kwa wajumbe wa Kamati ya PAC iliyowakutanisha wajumbe kutoka mataifa ya Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Malawi, Ujerumani na wadau wengine wa maendeleo, alieleza namna wabunge walivyoungana kwa ajili ya kutetea maslahi ya taifa bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Akizunguimzia mikakati mipya ya alisema kwamba kwa sasa wanatarajia kuipa nguvu zaidi ofisi yake na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ili aweze kukagua sio tu hesabu zinazowasilishwa na wataalamu katika makabrasha, bali kwenda hadi katika miradi husika na kufanya tathmini ya ubora wa miradi hiyo kwa kiwango cha fedha zinazotolewa.

Akizungumzia hilo, Utuoh alisema kwamba kwa sasa wanaangalia namna ya kuboresha zaidi ukaguzi kwa kuhakikisha kwamba kila mmoja anawajibika katika matumizi ya rasilimali za umma na kuzuia aina yoyote ya ufujaji.

“Kupitia utaratibu huu, tunataka kuona rasilimali za umma zinatumika kikamilifu katika kiwango kinachohitajika ili kuinua maisha ya watu,” alisema.

Utuoh hakusita kusisitiza kwa kutoa ushauri kwa Kamati ya Fedha na Uchumi kuwa bajeti imekuwa haiendi vyema kutokana na upungufu wa mapato huku mahitaji yakiwa makubwa kuliko kipato halisi.
Aliishauri kamati hiyo kuangalia namna ya kuongeza vyanzo vya mapato kwa Serikali kuliko kuendelea kutegemea vyanzo vilivyopo kwa sasa ili kuongeza mapato yanayokwenda sawa na mahitaji.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Anna Makinda alisema kwamba wanatarajia kuwapo mabadiliko makubwa katika suala la ukaguzi kwa kuhakikisha kila kinachofanywa kwa kutumia fedha za umma kinakuwa na thamani inayoendana na kiasi cha fedha hizo.

Alisema kwa sasa hakuna mzaha kwa watu wanaotumia vibaya fedha za umma na kwamba atahakikisha Bunge linakuwa na nguvu katika ukaguzi na wote wanaohusishwa na ubadhirifu wa mali za umma washughulikiwe upasavyo.

Pia alitoa onyo kwa watumishi wenye tabia ya kutoa vitisho kwa wabunge wanaosimamia hoja za kuwawajibisha wabadhirifu bungeni akisema kwamba tabia hiyo haitawasaidia kwa kuwa kwa namna yoyote ni lazima watawajibishwa upasavyo kwa matendo yao.

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: