Home > All Stories > Benki ya Wakulima yakaribia kuanza

Benki ya Wakulima yakaribia kuanza


SERIKALI imesema kuwa Benki ya Wakulima inatarajiwa kukamilika wakati wowote mwaka huu na kuanza kutoa mikopo mikubwa na ya muda mrefu ili kuboresha sekta ya kilimo nchini iliyo tegemeo kubwa katika kutoa ajira na kuongeza kipato cha wananchi wengi.
Aidha, serikali pia imekubali kuongeza mtaji kwenye Benki ya Rasilimali nchini (TIB) ili kuiwezesha kuwa na uwezo wa kutoa fedha zitakazotumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, ikiwemo ya uboreshaji wa miundombinu.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa 38 wa Taasisi za Benki za Maendeleo barani Afrika (AADFI) unaofanyika jijini hapa chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Peter Noni.
Mbene alisema kuwa, serikali imekubali kutenga kati ya dola za Marekani milioni 400 na 500 kwa ajili hiyo ambapo benki hiyo ya wakulima inatarajiwa kukamilika wakati wowote ndani ya mwaka huu kwani mchakato wake ulishaanza.
“Benki za maendeleo zina mtazamo wake, zinatoa mikopo mikubwa na ya muda mrefu kwa shughuli za kilimo, shule, ujenzi wa miundombinu na masuala ya mawasiliano, hivyo serikali imetafakari na imekubali kutoa fedha kwa ajili ya kuongeza mtaji TIB na nyingine zitatumika kwenye Benki ya Wakulima ambayo imekaribia kukamilika,” alisema Naibu waziri huyo wa fedha.
Akimkaribisha Mbene kufungua mkutano huo, Mwenyekiti wa AADFI, Noni alisema kuwa ujenzi wa majengo kwa makao makuu ya taasisi hiyo zilizoko Abidjan, Ivory Cost unaendelea vizuri na kuwataka wanachama wa taasisi hiyo kuendelea kuchangia kama walivyokubaliana.
Akizungumza kabla ya kufunguliwa warsha yao ya siku moja iliyofanyika juzi, Noni alizitaka nchi za Afrika kuziongezea mitaji benki hizo za maendeleo ili kuzijengea uwezo wa kuwasiliana na taasisi za fedha ndani na nje ya nchi, hivyo kuwa na fedha za kutosha kutumika kwenye uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambayo ni nguzo muhimu ya maendeleo.
Alisema kuwa suala la uboreshaji wa miundombinu kwenye nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania linahitaji kiasi kikubwa cha fedha, hivyo haliwezi kufanikiwa endapo serikali zitaendelea kutegemea mikopo ya benki kubwa za kimataifa na bajeti zao pekee, badala yake zimeshauriwa kushirikiana na benki za maendeleo zilizopo kwenye nchi zao.

CHANZO: http://www.freemedia.co.tz

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: