Home > All Stories > NSSF waidai Wizara bil. 14/- zilizojenga UDOM

NSSF waidai Wizara bil. 14/- zilizojenga UDOM

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeishitaki Wizara ya Fedha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, kwa kutolilipa Sh bilioni 14 ikiwa ni malipo ya awali ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi zaidi ya 5,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi wa shirika hilo kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 mbele ya kamati hiyo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi, Yacoub Kidula, alisema tayari shirika hilo limewasilisha malalamiko yake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.

Alisema shirika hilo liliingia mkataba wa ujenzi wa hosteli hizo mwaka 2007 na kukubaliana ujenzi uanze Oktoba mwaka huo na majengo hayo kukabidhiwa Serikalini Aprili 2009.

“Ilipofika Desemba 2007 Serikali ilibadilisha na kutaka ujenzi huo ufanyike kwa haraka na badala ya majengo hayo kukabidhiwa Aprili 2009, yakakabidhiwa Agosti 2008, jambo ambalo tulilikubali kwa masharti mawili,” alisema Kidula.

Alibainisha masharti hayo kuwa ni kuongezwa katika mkataba kiasi cha Sh bilioni 1.5 zaidi ya makubaliano ya awali ambayo yalikuwa mradi mzima Sh bilioni 35 na Serikali kuhakikisha kuwa inatoa kibali cha ujenzi wa haraka ifikapo Desemba 31, mwaka 2007.

Alisema pamoja na masharti hayo, Serikali haikutoa kibali cha kuharakisha ujenzi huo kama ilivyotakiwa na badala yake ilitoa kibali hicho Mei 2008 ikiwa imebaki miezi mitatu, majengo hayo yakabidhiwe kwa mujibu wa makubaliano mapya ya kuharakisha ujenzi huo.
Hata hivyo, Kidula alisema shirika hilo baada ya kuona Serikali inachelewa kutoa kibali hicho, ilitoa kibali bila idhini ya Serikali na kuruhusu mkandarasi aanze ujenzi Aprili 2008 na kukamilisha kazi na kuikabidhi Septemba 27, mwaka huo badala ya Agosti mwaka huo kama makubaliano yalivyokuwa.

“Tulipoanza kudai malipo yetu tukaambiwa kuwa hatupaswi kupewa fedha yeyote kwa kuwa hatukukamilisha kazi kwa muda muafaka wakati ukweli ni kwamba wizara yenyewe ilichelewesha kutoa kibali cha kuharakisha ujenzi huu ndio maana hatukusaini nyongeza ya malipo haya,” alisema.

Naye Meneja wa Miradi wa shirika hilo, John Msemo, akizungumzia utekelezaji wa miradi iliyo chini ya NSSF, alisema mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni tayari mkataba wa utekelezaji wake umesainiwa Januari mwaka huu na unatarajiwa kujengwa kwa miezi 36 hivyo kukamilika mwaka 2015.

Aidha, alisema kwa sasa shirika hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya ongezeko kubwa la mafao ya kuacha uanachama jambo ambalo litasababisha wastaafu miaka ijayo kukosa sifa ya kupata pensheni hivyo taifa kuwa na wazee wasio na kipato.

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: