Home > All Stories > Wanakijiji waung’oa uongozi wao

Wanakijiji waung’oa uongozi wao

WANAKIJIJI wa Siuyu wilaya mpya ya Ikungi wametishia kuuondoa madarakani uongozi wa serikali ya kijiji chao kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za michango ya wananchi.

Tishio la wanakijiji hao lilitolewa wakati wa mkutano wa hadhara uliosimamiwa na kundi la askari wa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Singida baada ya wanakijiji hao kuwataka viongozi hao waondoke kwanza.

Viongozi wanaokataliwa ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Serafini Njera na wajumbe ambao ni Mikaeli Ghuliku, Joseph Daniel, Protasi Cosmasi, Alfred Marco, Potami Dule, Rozimary Ramadhani, Salumu Alli, Evalina Emil na Lazaro Gaspari.

Wengine ni Stephano Federiko na Zainabu Jumanne, Halima Rajabu, Marcelina Agustino, Juma Omari, Mateo Senge, Maria Evarist, Evarist Mkhotya, Veronika Simon, Teotim Serafin, Winfrida Hongoa, Mayasa Juma, Anjelina Nyambi na Marco Muna.

Licha ya kuukataa uongozi huo mkutano ulimalizika bila muafaka chini ya ulinzi wa askari wa kutuliza ghasia (FFU) baada ya Ofisa Tarafa ya Mungaa William Swai kuwasomea wanakijiji hao barau iliyokuwa na tuhuma za viongozi hao.

Sehemu ya barua hiyo ilieleza kwamba viongozi hao hawana ushirikiano na wanavijiji huku wakituhumiwa kwa ubadhirifu huku askari mstaafu na mkazi wa kijiji hicho Onesmo Msuta akieleza namna alivyokamata magari 84 yenye miti ambayo ushuru wake ni sh 33,060,000 ambazo hazijulikani zilipo.

Baada ya maelezo ya wananchi mbalimbali kuhusu tuhuma za viongozi hao na mapendekezo ya kuundoa madarakani uongozi uliopo ili kupisha uchaguzi mdogo walikubaliana kuifunga ofisi ya kijiji hadi watakapokubaliwa kufanyika kwa uchaguzi mdogo kujaza nafasi hizo.

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: