Home > All Stories > Watumishi 11 wasimamishwa kazi Sengerema

Watumishi 11 wasimamishwa kazi Sengerema

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wamewasimamisha kazi watumishi 11 na kuiagiza tume ya uchunguzi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa kuwawajibisha watumishi hao.

Waliosimamishwa ni Elikalia Edward, Mohamed Kabelwa, Lameck Butoto, Onesmo Bilago, Sifaeli Mwiguli na mweka hazina aliyetajwa kwa jina moja la Deus.

Wengine ni Thomas Mwenda, ofisa ardhi wilaya aliyetajwa kwa jina moja la Mnyeti, Paphil Mashashua, na aliyekuwa ofisa ugavi aliyetajwa kwa jina moja la Lugakila.

Watumishi waliosimamishwa ni kati ya 25 waliotakiwa kujieleza ndani ya siku 14 mbele ya kamati ya maadili ya madiwani na kwamba shutuma hizo zinatokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyobaini kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo wilayani hapa.

Kikao kilichowasimamisha kazi watumishi hao kiliongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mathew Lubongeja kuanzia saa moja asubuhi hadi saa mbili usiku huku wakiwatimua waandishi wa habari wakati wa kikao hicho.

“Niacheni, sitaki….si mmepata taarifa? Aaah nawahi kikao Chato usiku huu niacheni. Sasa ngojeni niwaambie tumewasimamisha watumishi 11 kati ya wale 25 waliotakiwa wajieleze kwenye kamati ya maadili,” alisema Lubongeja ambaye hakupenda kuzungumza na vyombo vya habari.

Watumishi waliosimamishwa walikuwa kwenye Idara ya Fedha, Sheria, Mipango, Ardhi, Maji, Ujenzi, Kilimo, Maendeleo ya Jamii na Ugavi wakati afya haikuwa na kasoro.

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: