Home > All Stories > Mwanafunzi Veta kortini kwa wizi wa Sh20 milioni

Mwanafunzi Veta kortini kwa wizi wa Sh20 milioni

 

MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi Veta wa jijini Dar es Salaam, Zuhura Seif (20) amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka  mawili likiwemo la  wizi wa Sh20  milioni mali ya Nuru John.

Mwendesha mashtaka wa mkaguzi wa Polisi, Denis Mujumba alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo  Juni 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mujumba alidai siku hiyo ya tukio saa 7:00 mchana katika eneo hilo mshtakiwa aliiba mikufu miwili na hereni  nne za dhahabu  vyote vikiwa na thamani ya Sh 20 milioni mali ya Nuru John.

Mshtakiwa alikana shtaka na hakimu Ester Mwakalinga aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, mwaka huu itakapotajwa tena.  Mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakao saini nusu ya mali iliyoibwa.  Katika kesi nyingine, Tazan Richard (18) amefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shtaka la kujeruhi.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 14 mwaka huu mtaa wa Libya.  Katuga alidai siku hiyo saa 4:45 usiku katika eneo hilo, mshtakiwa alimjeruhi Richard Aloyce kwa kumpiga kwa fimbo machoni na kumsababishia majeraha.  Mshtakiwa alikana shtaka na hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joyce Minde aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 4 mwaka huu itakapotajwa tena.

CHANZO: http://www.mwananchi.co.tz/

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: