Home > All Stories > Tuliwakumbusha, CCM wajihadhari na ‘fedha za bhangi’, lakini hawakusikia

Tuliwakumbusha, CCM wajihadhari na ‘fedha za bhangi’, lakini hawakusikia

 

SIKU zote Waswahili wanasema: “Msemea sikioni siyo majinuni!” Hata hivyo, ni wachache wanaoweza kuzingatia yale wanayoambiwa na daima wanapoyafanyia kazi huwa wanapata matokeo mazuri.

Suala la rushwa ndani ya Chama cha Mapinduzi limekuwa sugu, wenye fedha wamekuwa wakilangua kura ili kupata uongozi, hata kama hawana sifa stahiki. Lakini pamoja na ‘Wenye hekima wa Babeli’ kutahadharisha madhara ya mchezo huo mchafu, bado wahusika wameziba masikio kwa nta, hawataki kusikia la Muadhini wala Mnadi Swala!

Matokeo yake CCM limekuwa kokoro kama alivyopata kusema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Kokoro linalovua samaki na konokono kwa pamoja, na inahitajika busara na hekima kuweza kuchambua samaki na konono hao ambao ni hatari mno.

Uongozi ndani ya CCM ni sawa na kutangaza zabuni, ambayo mwenye fedha nyingi ndiye anayeshinda na kupewa uongozi huo. Rushwa imekuwa kansa mbaya ndani ya CCM, fedha zinamwagwa nje nje na viongozi wao wanaangalia na kuchekelea, wanakemea rushwa na tabasamu pana kana kwamba ni kitu cha kawaida tu. Hii ni aibu kwa chama kikongwe na chenye dhamana ya kuongoza Taifa!

Mwanzoni mwa chaguzi za CCM tukaonya tena, kwamba CCM wajihadhari na ‘fedha za bhangi’. Wengine tuliona, tukasikia, hivyo tukaamua kuwakumbusha tu, kwamba tayari fedha chafu zimekwishamwagwa kuanzia ngazi za chini za kuwania uongozi ndani ya chama hicho.

Ifuatilie zaidi…www.kwanzajamii.com/?p=4111

 

Advertisements
Categories: All Stories
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: