Tusipoangalia tutaibinafsisha Serikali

November 21, 2012 Leave a comment

Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye utawala wake ndio unaotajwa kutekeleza ‘kwa vitendo’ sera ya ubinafsishaji.

 

Na Daniel Mbega

 

BADO najiuliza bila kupata jibu sahihi kuhusiana na Sera ya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ya mwaka 1992 ambayo ilishuhudia mabadiliko katika mashirika 400 yaliyogawanywa katika makundi matatu makuu – mashirika Read more…

Advertisements
Categories: All Stories

Biashara ilivyofuta Utakatifu Ikulu

November 18, 2012 Leave a comment

 

 

Na Daniel Mbega

 

SIYO siri kwamba, viongozi wetu wa sasa wa Serikali wamechafuka, wameoza na kuvunda kutokana na kukosa uadilifu na uaminifu. Rushwa imetamalaki kila kona, wengi wametumia na wanaendelea kutumia vyeo vyao, ambavyo ni dhamana, kujilimbikizia mali.

Jinsi wanavyopigana vikumbo kila mahali kuusaka uongozi ni dalili pekee kwamba, Read more…

Categories: All Stories

Von Zelewiski auawa kwa kupigwa nyundo

November 8, 2012 Leave a comment

HUU ni mfululizo wa Makala ya Uchunguzi kuhusiana na historia ya kiongozi mkuu wa Wahehe, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Kilonge Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, kama yanavyoandikwa na Mwandishi Wetu DANIEL MBEGA, ambaye amefanya uchunguzi kwa takriban miezi mitatu sasa katika kuhimiza utalii wa ndani na kuhifadhi historia yetu. Endelea na Sehemu hii ya Sita…

 

HADI wakati huo, tayari von Heydebreck – mmoja wa manusura katika vita hivyo – alikuwa amekwishajeruhiwa na kuanguka akiwa amepoteza fahamu, lakini baadaye aliandika kwenye ripoti yake: “…Mfululizo wa matukio hadi wakati huu ulikuwa umetumia dakika mbili au tatu tu. Nilitambua hilo kabla ya kujeruhiwa, Wasudani tayari walikuwa wamekimbia kurudi nyuma vichakani baada ya kufyatua risasi mara mbili hivi. Mimi na askari wa Kikosi cha Tano tulilazimika kujilinda na kujitetea baada ya kuona Wahehe wakija katika umbali wa hatua 30. Kama sikosei, Read more…

Categories: All Stories

Tuliwakumbusha, CCM wajihadhari na ‘fedha za bhangi’, lakini hawakusikia

November 8, 2012 Leave a comment

 

SIKU zote Waswahili wanasema: “Msemea sikioni siyo majinuni!” Hata hivyo, ni wachache wanaoweza kuzingatia yale wanayoambiwa na daima wanapoyafanyia kazi huwa wanapata matokeo mazuri.

Suala la rushwa ndani ya Chama cha Mapinduzi limekuwa sugu, wenye fedha wamekuwa wakilangua kura ili kupata uongozi, hata kama hawana sifa stahiki. Lakini pamoja na ‘Wenye hekima wa Babeli’ kutahadharisha madhara ya mchezo huo mchafu, bado wahusika wameziba masikio kwa nta, hawataki kusikia la Muadhini wala Mnadi Swala!

Matokeo yake CCM limekuwa kokoro kama alivyopata kusema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Kokoro linalovua samaki na konokono kwa pamoja, na inahitajika busara na hekima kuweza kuchambua samaki na konono hao ambao ni hatari mno.

Uongozi ndani ya CCM ni sawa na kutangaza zabuni, ambayo mwenye fedha nyingi ndiye anayeshinda na kupewa uongozi huo. Rushwa imekuwa kansa mbaya ndani ya CCM, fedha zinamwagwa nje nje na viongozi wao wanaangalia na kuchekelea, wanakemea rushwa na tabasamu pana kana kwamba ni kitu cha kawaida tu. Hii ni aibu kwa chama kikongwe na chenye dhamana ya kuongoza Taifa!

Mwanzoni mwa chaguzi za CCM tukaonya tena, kwamba CCM wajihadhari na ‘fedha za bhangi’. Wengine tuliona, tukasikia, hivyo tukaamua kuwakumbusha tu, kwamba tayari fedha chafu zimekwishamwagwa kuanzia ngazi za chini za kuwania uongozi ndani ya chama hicho.

Ifuatilie zaidi…www.kwanzajamii.com/?p=4111

 

Categories: All Stories

Mwanzo wa mapigano, Wajerumani wafyekwa

August 8, 2012 Leave a comment

HUU ni mfululizo wa Makala ya Uchunguzi kuhusiana na historia ya kiongozi mkuu wa Wahehe, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Kilonge Mwamuyinga, maarufu kama Mkwawa, kama yanavyoandikwa na Mwandishi Wetu Read more…

Categories: All Stories

Mkwawa awatisha Wajerumani

August 8, 2012 1 comment

Askari wa Kihehe.

Na Daniel Mbega

BAADA ya kufanikiwa kuurejesha utawala kwenye himaya yake mwaka 1890 kufuatia kumtwanga Mwamubambe Mwalunyungu aliyekuwa na Read more…

Categories: All Stories

Utawala wa Munyigumba wapinduliwa na mkwewe

July 26, 2012 1 comment

Na Daniel Mbega
UTAWALA wa Munyigumba Kilonge Mwamuyinga ulidumu kwa muda wa miaka 19 tangu alipomuua kaka yake Ngawonalupembe mwaka 1860.
Mtwa Munyigumba alifariki mwaka 1879 Read more…

Categories: All Stories