Bosi Bodi ya Pamba apigwa ‘stop’


WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini Michael Ntunga kwa tuhuma za kuwahujumu wakulima wa zao hilo.

Chiza ambaye ni Mbunge wa Buyungu alitoa uamuzi huo jana alipozungumza na wakazi wa jimbo lake na kusema uamuzi huo utasaidia uchunguzi huru wa tuhuma za uhujumu wa zao hilo zinazotolewa na wabunge.

Aidha waziri huyo ameahidi kumchukulia hatua za kisheria mkurugenzi huyo iwapo atakutwa na makosa yakiwemo ya kufuja fedha za fidia za wakulima wa pamba zilizotolewa mwaka 2009 na serikali na kusababisha zao hilo kushuka bei baada ya kuyumba kwa soko la dunia.

Tuhuma nyingine zinazomkabili Ntunga ni kushindwa kusimamia usambazaji wa dawa za kuua wadudu waharibifu wa pamba ambapo msimu huu dawa hizo hazikuua wadudu hali iliyoibua malalamiko kwa wakulima.

Ntunga alidaiwa kupitisha madai ya malipo ya sh milioni 50 kwa kampuni itakayonunua zao hilo kwa kila kanda jambo lililopingwa kwa maelezo kwamba ni kumkandamiza mkulima kinyume cha uanzishwaji wa bodi hiyo.

Published by mbega2011

I am a Tanzanian Investigative Journalist with specialization in Agriculture, Tourism and Environmental advocacy, Transparency and Accountability. I like positive changes and don't like people who don't do nothing in their respective positions. I don't like people who temper with environment.

Leave a comment